Mtoto mwenye kipaji cha ajabu nchini Kenya, amshangaza Alicia Keys (+video)
Mtoto mmoja nchini Kenya aliyetambulika kwa jina la Gracious Amani amejikuta akitajwa na msanii mkubwa wa muziki Duniani, Alicia Keys baada ya video yake inayomuonesha akiimba wimbo wa ‘Girl On Fire’ kusambaa nchini Kenya. Video ya mtoto huyo ilianza kusambaa kwa kasi mwanzoni mwa mwezi huu nchini Kenya ambapo Amani alionekana akiimba kwa ustadi mkubwa wimbo wa ‘Girl On Fire’ wa Alicia Keys kitu ambacho kiliwavutia mamilioni ya watu nchini Kenya. Ukweli ni kwamba Alicia Keys naye amemsikiliza mtoto huyo na kuposti video ya mtoto huyo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na kuandika “Look at this beautiful soul!! SHINE!!!!“. Kwa mujibu wa mahojiano aliyoyafanya mtoto huyo na kituo cha runinga cha NTV cha nchini Kenya, Amani anatoka Githurai jijini Nairobi na Baba yake ni muandaaji wa muziki. Maoni ya watu wengi waliokomenti kwenye posti hiyo ya Alicia Keys wanamtaka amsaidie mtoto huyo kwa hali na mali ili aweze kutimiza ndoto zake. alagardienI say yo