Posts

Showing posts from May 31, 2018

Diamond Akana Kumpigia Magoti Zari ili Warudiane

Image
Msanii wa bongo fleva maarufu  nchini , Diamond Platinumz kwa mara ya kwanza amefunguka na kuzungumzia swala lake la kuachana na Zari na kumuomba radhi mwanamama huyo ambapo taarifa za hapo awali ziliwahi kusema kuwa kwa sasa Diamond amekuwa akipiga safari nyingi za Afrika ya Kusini ili kuomba radhi  kwa mwanamke huyo. Akizungumzia kuhusu vijembe vingi ambavyo diamond amekuwa akitupiwa na mwanamama huyo hasa vya hapa karibuni alipokuwa kenya, Diamond alisema ; "hayo ya kenya bwana tuachane nayo, mimi nadhani yameshapita naomba tuendelee na  haya yasasa itapendeza sana” Hata hivyo, mwandishi hakuishia hapo ndipo alipoamua kumuuliza moja kwa moja kuhusu yeye kusafiri kwenda afrika ya kusini kwa ajili ya kuomba radhi kwa zari huku akienda kwa siri mara kwa mara na diamond alijjibu kuwa safari zake za afrika ya kusini hazihusiani na mambo hayo. "N kweli ninaenda na so mara moja au mara mbili nimekuwa ninaenda,nakwenda kule sio kwa ajili ya kumuomba msamaha , h

Belle 9 Akana Tetesi za Kukimbia Mjini Baada Ya Kufulia

Image
Msanii mkongwe wa Bongo fleva aliyewahi kutamba na kibao chake cha ‘Masogange’ Belle 9 amekana tetesi zinazodai kuwa amefulia. Belle 9 alipata shavu la kusainiwa na label ya ‘Vitamin Music’ ambayo ilimuhamisha kutoka Morogoro na kumleta Dar kwa ajili ya kufanya Muziki lakini baada ya kuoa  Belle 9 alipotea kidogo. Baadae zilizuka stori kuwa Belle 9 ameamua kurudi nyumbani Morogoro kutokana na kukosa shoo na kufulia hapa Dar kiasi ya kwamba ana kosa hata pesa ya kulipia kodi ya nyumba. Kwenye Interview aliyofanya na Enews ya East Africa Tv, Belle 9 amekana tetesi hizo za kufulia na kusema hajahama Dar bado yupo mjini: "Dah Hapana muda mrefu sijafika Morogoro mi Nipo Dar, hizo ni rumors tu zinazosambazwa na watu Lakini pia naona wanasema hivyo kwa sababu sionekani Kwenye maeneo ya starehe mengi." Belle 9 amerudi upya na kazi yake mpya aliyotoa siku chache zilizopita inayokwenda kwa jina la ‘Dada’.

Mpoki apewa shavu na Alikiba

Image
Katika kuelekea mchezo maalumu wa hisani ya kuchangia elimu, msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba ametangaza kikosi cha wachezaji watakao kuwa upande wake kupambana dhidi ya  kikosi cha wachezaji watakaokuwa upande wa mshambuliaji wa timu ya Taifa na klabu ya KRC Genk, Mbwana Samatta. Kwenye kikosi hicho, Alikiba amemchukua mshambuliaji hatari wa klabu ya Simba, Emmanuel Okwi na wachezaji wengine kama John Bocco, Msuva, Erasto Nyoni, Abdu Kiba na wengineo kama inavyoonesha hapa chini kwenye picha. Kikubwa zaidi ni kwamba Alikiba amemchagua mchekeshaji maarufu nchini Tanania, Mpoki kuwa msemaji wa timu yake aliyoichagua.

Nuh Mziwanda Azungumzia Picha Zake Tata na Amber Lulu

Image
Msanii wa muziki wa bongo fleva Nuh Mziwanda amaefunguka na kuzungumzia video tata iliyokuwa ikiwaonyesha yeye na msanii mwenzake wa kike Amber  lulu wakiwa sehemu faragha  wakiwa katika mapozi ya kimahaba. Wawili hao wanasadikika kuwa wapenzi hasa baada ya kuonekana kwa vido hiyo ambayo ilisambaa kupitia snap chat ya Amber Lulu. Kwa mujibu wa Nuh anasema kuwa hakuna chochote kinachoendelaa kimapenzi kati yao bali kuna project wameeianda kati yao na ile iliyovuja walikuwa location kwa ajili ya ku-shoot. "Mimi na Amber tuna project na hakuna kitu chochote, ila mimi niko snap chat kwaio wakati tunashoot video kulikuwa na zile vibes za snapchat  za kucheka, ku-enjoy na kufanya mambo mengine mengi , yeye alikuwa akichukua kwenye sanap na mimi nilikuwa nachukua katika snap lakini haikuwa kwa ubaya, na wala sikumwambia aitoe maana pale ile ni snapchat yake."

Wema Sepetu Aenda Kufanyiwa Upasuaji India

Image
Msanii Wema Sepetu anayekabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo May 29, 2018 ili kujitetea katika kesi yake kwa sababu amekwenda nchini India kufanyiwa upasuaji. Hayo yameelezwa na Mama mzazi wa Wema, Mariam Sepetu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa serikali, Constantine Kakula kuhoji kwanini Wema hakufika mahakamani. Wakili Kakula amedai kuwa anashangaa kutokumuona Wema, kwani hata ahirisho la mwisho la kesi yake hakuwepo. Baada ha kueleza hayo, Mama Wema akatoa nyaraka za Wema za kusafiria na kuieleza mahakama kuwa Wema anaumwa na amekwenda nchini India kufanyiwa upasuaji. Wakili Kakula amedai kuwa hakuna uthibitisho wowote wa kuonyesha Wema anaumwa, hivyo anaiomba mahakama isimamie sheria. Kutokana na hoja hiyo, Hakimu Simba amesema ni kweli hakuna uthibitisho, hivyo katika tarehe ijayo uthibitisho unapaswa kuwepo, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi June 13,2018. Mbali na

Rayvanny " Rosa Ree is my Favorite Wangu Katika Marapa wa Kike"

Image
Msanii wa muziki Bongo kutoka WCB, Rayvanny ameeleza ni kwanii Rosa Ree ndiye rapper pekee wa kike katika remix ya ngoma yake ‘Pochi Nene’ Muimbaji huyo amesema kuwa kwanza amekuwa akivutiwa na muziki wa Rosa Ree, pili wimbo wenyewe ulimuhitaji Rosa Ree kutoka na aina yake ya rap. “Nawakubali wasichana wote wanaorap lakini Rosa Ree is my favorite wangu naweza kusema lakini niliona kama atafaa zaidi kutokana na concept ya wimbo wenyewe,” amesema. “Ukimsikia anavyo-sound kama Nicki Minaj sio Nicki Minaj, nikaona kwenye biti kama lile ataleta vibe na ndio maana nikaamua kumuweka,” Rayvannuy ameiambia Wasafi TV. Poch Nene Remix imewakutanisha wasanii kama Khaligraph Jones, Godzilla, Rosa Ree, Izzo Bizness, Country Boy, Young Dee na Wakorinto.

Mama Wema Sepetu Asema Mtoto Wake Yupo India Kwa Matibabu

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuendelea na kesi inayomkabili staa wa filamu nchini, Wema Sepetu,  anayekabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya ambapo ameshindwa kufika katika mahakama hiyo leo Mei 29, mwaka huu,  kwa ajili ya kuendelea kujitetea katika kesi yake ya matumizi ya dawa za kulevya kwa madai kwamba amekwenda nchini India kufanyiwa upasuaji. Hayo yameelezwa leo na mama mzazi wa staa huyo, Miriam Sepetu,  mbele ya hakimu, Thomas Simba, baada ya Wakili wa Serikali, Constantine Kakula, kuhoji kwa nini Wema hakufika mahakamani. Wakili huyo  amedai kuwa anashangaa kutomuona Wema, kwani hata ahirisho la mwisho la kesi yake hakuwepo. Baada ya kueleza hayo, Mama Wema akatoa nyaraka za Wema za kusafiria na kuieleza mahakama kuwa Wema anaumwa na amekwenda nchini India kufanyiwa upasuaji. Wakili Kakula amesema kuwa hakuna uthibitisho wowote wa kuonyesha Wema anaumwa, hivyo akaiomba mahakama isimamie sheria. Kutokana na hoja hiyo, Hakimu Simba amesema

Amber Lulu Afunguka Kuhusu Video yake na Nuh Mziwanda Iliyovuja Wakifanya yao

Image
Msanii wa bongo fleva na muuza nyago katika video za wasanii Amber Lulu amefungukia video inayosambaa mitandaoni ikimwonyesha yeye na msanii mwenzake Nuh mziwanda wakiwa katika pozi za kimahaba.  Amber Lulu amesema video hiyo imetokana na nyimbo yao mpya watakao uachia hivi karibuni na wala hana uhusiano wowote wa kimapenzi na Nuh Mziwanda huku akidai kuwa video hiyo imemsababishia ugomvi na mpenzi wake ambaye ni msanii wa Kenya, Prezzoo.  VIDEO:

Uwoya adaiwa ndio chanzo cha Dogo Janja kuwa na muonekano wa kike

Image
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dogo janja ambaye sasa hivi ameachia video ya wimbo wake mpya wa 'Wayu wayu' na kuacha gumzo kwa mashabiki kwa kuvaa uhusika wa mwanamke, na kusema kuwa mke wake ndiye alimfanya awe hivyo. Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dogo Janja amesema mke wake ambaye ni muigizaji wa filamu za bongo, Irene Uwoya, ndiye alianza kumfanyia make up wakiwa mapumzikoni Zanzibar, na kumvalisha vitu vya kike, ndipo walipopata idea ya kufanya video akiwa kama mwanamke. “Mke wangu kabla sijaanza kushoot alianza kunifanyia make up na kunivesha vesha tulipokuwa vacation (mapumzikoni) Zanzibar, akawa ananicheka, mpaka siku tunaenda kushoot ile make up ilibidi anifanyie yeye lakini ilitokea dharula hakuwepo, akaniambia niende kwa mtu anifanyie make up ya nude mimi hata siijui, hata lile wigi alinipa mke wangu na mimi nikapita nalo”, amesema Dogo Janja. Kitendo cha Dogo Janja kuigiza kama mwanamke kimeonekana kuwakwaza watu wengi

Amber Lulu Ametaja List ya Mastaa wote Bongo Aliowahi Kutoka nao

Image
Muimbaji wa Bongofleva Amber Lulu leo kupitia mahojiano yake na kipindi cha Break cha Clouds TV amekuwa gumzo mitandaoni baada ya kukubali kuweka wazi orodha ya mastaa wa Bongo ambaye amewahi kutoka nao kimapenzi. Amber Lulu akihojiwa na Simple The Boy aliulizwa vipi anatoka kimapenzi na Nuh Mziwanda na alikanusha  lakini alipoulizwa  ni mastaa gani wa bongo ambao amewahi kuingia nao katika mahusiano ya kimapenzi alikuwa radhi kusema.

MSAMI “Nilivyoachana na Uwoya Nilikuwa Bado Nampenda”

Image
Jana May 30, 2018 kupitia kipindi cha XXL cha Clouds Fm dancer na pia msanii wa Bongofleva  Msami alifanya mahojiano na kuongea vitu kibao ikiwemo mahusiano yake na muigizaji Irene Uwoya ambaye kwa sasa ni mke halali wa Dogo Janja. Msami amefunguka na kusema kuwa Godzilla aliwahi kumpigia simu aliyekuwa mpenzi wake Irene Uwoya na kumzungumzia vibaya juu yake na hakujua lengo halisi la Godzilla kufanya hivyo ilikuwa ni nini hasa. “Wakati nikiwa na mahusiano na Irene Uwoya Godzilla alimpigia simu uwoya na kunipondea sana” Msami ameongezea pia na kusema kuwa wakati anaachana na Irene Uwoya alikuwa bado anampenda.

VIDEO: Nitaolewa Mungu Akinipa Mume Nina Hisia na Mimi, Diamond Atasubiri - Queen Darleen

Image
Msanii kutoka lebo ya WCB ambae pia ni Dada wa Diamond Platnumz, Queen Darleen ambae ametamba na ngoma ya Touch ambayo imetengezwa na studio ya Wasafi, amesema kuwa yeye pia ana hisia na upendo na anapenda hivyo kuhusiana na yeye kuwa na ndoa Ataolewa hadi mungu atakapompatia, na Diamond atasubiri sana hadi yeye aolewe.  TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI:

Chuchu Hans Atema Nyongo Kuishi na Ray Wakati wa Mfungo wa Ramadhani

Image
MUIGIZAJI wa kitambo Bongo Muvi, Chuchu Hans amefunguka kuwa watu wanaomhukumu kuwa anakosea kuwa karibu na mzazi mwenziye ambaye ni muigizaji pia, Vincent Kigosi ‘Ray’ wakati huu wa mfungo wa Ramadhani na yeye ni Muislamu waache kwani wao siyo Mungu. Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu akiwa nchini Afrika Kusini na mzazi mwenziye huyo kwa ajili ya kushuti filamu, alisema kuwa kuishi na mzazi mwenziye huyo kwa ajili ya kazi haoni kama ni dhambi lakini anashangaa watu wanavyotoa hukumu mitandaoni kwamba anakosea. “Mimi ninachojua wa kumhukumu mtu ni Mungu pekee kwa sababu yeye ndiyo anajua ukweli wote na anajua kila kitu cha binadamu na si mtu mwingine, najua nilivyo huku na Ray watu wanasema sana tu lakini sijali,” alisema Chuchu

Mastaa Hawa Wafuatao Wametoka Relini..Ukali wao Wapungua

Image
KUTOKA relini ni moja kati ya misemo inayotumiwa sana na watoto wa ‘dijitali’ ikiwa na maana kuwa juu na ghafla kupotea. Kutoka relini huku inawezekana ulikuwa na pesa na baada ya kipindi ukawa huna kitu au unaweza kutamba kwa muda f’lani kwenye gemu na baada ya kipindi ukawa husikiki kama ilivyokuwa awali. Katika muziki wa Bongo Fleva nao kuna wasanii ambao wametoka relini. Walikuwa wakitamba na kukubalika kila wakitoa nyimbo zao lakini kwa sasa Tangu mwaka uanze, ameshatoa ngoma kibao zikiwemo Amsha Popo, Kaa Mbali Nao na Mikono Juu lakini bado zimemtoa nje ya reli. WEUSI Huwezi kutaja makundi ya Muziki wa Hip Hop Bongo ukaacha kulitaja Kundi la Weusi kutoka Arusha likiwa na vichwa ‘hatari’ kama vile Nikki wa Pili, Joh Makini pamoja na G Nako. Ngoma zilizow-aweka relini ni Gere, Nusu Nusu na Nje ya Box.Wakali hawa kwa muda mrefu wameweza kuteka Muziki wa Hip Hop Bongo na kufanya shoo kibao za ndani ya nchi. Walianza kutoka relini taratibu baada ya kuachia Ngoma