Mambo ni Hivi! Muigizaji wa Nigeria Kufunga Ndoa na Mdoli wa Ngono
Muigizaji wa Nigeria na mchekeshaji Benjamin Nwachukwu, anayejulikana na mashabiki wake kwa jina Shuga Shaa, amezua mjadala katika mji wa Lagos kwa kusema kwamba ana uhusiano na mwanasesere wa ngono kwa jina Tonto Shaa.
Mwanasesere huyo mrembo ana nywele bandia, kucha zilizotengezwa vizuri na huvalia vito pamoja na marashi ya bei ghali- na sasa pia ana gari lake.
Shuga Shaa alionekana akienda kutazama filamu ndani ya gari lake na mpenzi wake mpya.
Baadhi ya mashabiki wake walisikitishwa na kumtaja kuwa 'mwenda wazimu' na mtu 'aliye na tatizo la kiakili'.
Comments
Post a Comment