Sababu za kuachiwa Hamis Shaban Taletale maarufu kama Babu Tale mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Tip Top Connection, aliyekuwa akisota mahabusu, akisubiri amri ya kupelekwa kifungoni gerezani, zimebainika. Babu Tale ambaye pia ni meneja wa mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul, ‘Diamond Platnumz’, aliachiwa kwa muda na Jaji Edson Mkasimongwa, kwa kile kilichoelezwa kuwa amri ya kumkamata yeye na ndugu yake Idd Shaban Taletale ilitolewa kimakosa. Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka mahakamani hapo, makosa yaliyobainika katika amri hiyo ni kwamba aliyeitoa, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam, Wilbard Mashauri hakuwa na mamlaka ya kutoa amri hiyo na kwamba ilikuwa haieleweki. Hivyo Jaji Mkasimongwa alimwachia jana kwa muda lakini akamtaka afike mahakamani saa 6:00 mchana, leo Mei 25, 2018. Babu Tale alitiwa mbaroni Jumanne Mei 22, 2010, kwa amri ya mahakama hiyo iliyotolewa na Naibu Msajili Mashauri Februari 16 na hati ya kuwakamata iliyotolewa