Mtoto mwenye kipaji cha ajabu nchini Kenya, amshangaza Alicia Keys (+video)
Mtoto mmoja nchini Kenya aliyetambulika kwa jina la Gracious Amani amejikuta akitajwa na msanii mkubwa wa muziki Duniani, Alicia Keys baada ya video yake inayomuonesha akiimba wimbo wa ‘Girl On Fire’ kusambaa nchini Kenya.
Video ya mtoto huyo ilianza kusambaa kwa kasi mwanzoni mwa mwezi huu nchini Kenya ambapo Amani alionekana akiimba kwa ustadi mkubwa wimbo wa ‘Girl On Fire’ wa Alicia Keys kitu ambacho kiliwavutia mamilioni ya watu nchini Kenya.
Ukweli ni kwamba Alicia Keys naye amemsikiliza mtoto huyo na kuposti video ya mtoto huyo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na kuandika “Look at this beautiful soul!! SHINE!!!!“.
Kwa mujibu wa mahojiano aliyoyafanya mtoto huyo na kituo cha runinga cha
NTV cha nchini Kenya, Amani anatoka Githurai jijini Nairobi na Baba
yake ni muandaaji wa muziki.
Maoni ya watu wengi waliokomenti kwenye posti hiyo ya Alicia Keys wanamtaka amsaidie mtoto huyo kwa hali na mali ili aweze kutimiza ndoto zake.
Maoni ya watu wengi waliokomenti kwenye posti hiyo ya Alicia Keys wanamtaka amsaidie mtoto huyo kwa hali na mali ili aweze kutimiza ndoto zake.
- alagardienI say you should go hunt her down and change her life @aliciakeys, cos if I could I would have “WOW”
- joselopes502wish…could help her to be come a professional singer…
- diana.mac.omoloThanks for responding… @aliciakeys… That is a Kenyan upcoming star… Happy you took your time for thisπ
- true_north_stained_glassTHIS girl is on fire!!! WOW ππ₯π₯ And that sweet smile at the end π
- kakudeeI am proud of this young Queen and thanks @aliciakeys for sharing this there are so much untapped talent here in Kenya. Shine girlπππ
Comments
Post a Comment