Harmonize Atoboa Siri ya Ugumu Uliopo Ndani ya WCB
Msanii wa muziki Bongo, Harmonize ametaja ugumu uliopo ndani ya label ya WCB.
Harmonize ambaye anatamba na wimbo DM Chick amesema ugumu uliopo WCB ni kila msanii ana uwezo mkubwa, hivyo kila mmoja anahakikisha anafanya kazi nzuri.
“Ugumu ni pale ambapo unafanya kazi na wasanii wote ambao ni talented, so way competion katika kurekodi ngoma kila mtu anataka kutoa ngoma yake kali kumshinda mwenzake, so ugumu unaanzia hapo,” Harmonize ameiambia Planet Fm.
Utakumbuka kuwa Harmonize ndiye msanii wa kwanza kusainiwa katika label ya WCB ambapo kwa mara ya kwanza alitoa wimbo uitwao Iyola uliomtambulisha katika Bongo Flava. Baada yake ndipo wakafuata wengine kama Rayvanny, Rich Mavoko, Queen Darleen, Lava Lava na Mbosso.
Comments
Post a Comment