Spika Ndugai: Wizara Ya Fedha Ijitathmini
Spika wa Bunge, Job Ndugai ameitaka Wizara ya Fedha na Mipango, ijitathmini baada kushindwa kupeleka kwa wakulima wa korosho fedha za tozo za mauzo ya nje ya zao hilo. Akizungumza bungeni jijini Dodoma leo Mei 24, amesema kinachofanywa na wizara hiyo hakiwezi kukubaliwa kwa sababu kinaathiri zao la korosho nchini alipokuwa akijibu mwongozo wa kutaka kuahirisha bunge ulioombwa na Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) aliyetaka bunge lisitishe shughuli zake na kujadili suala la serikali kutotoa fedha hizo kwa wakulima wa korosho. Nape amesema: “kutopelekwa fedha hizo kumesababisha bei ya mbolea aina ya sulphur kupanda kutoka Sh 16,000 hadi 75,000”. Akiunga mkono hoja hiyo Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) amesema kutopelekwa kwa fedha hizo kunatokana na utaratibu wa serikali ya awamu ya tano kutofuata sheria zinazopitishwa na bunge. Akijibu miongozo hiyo, Spika Ndugai amesema suala hilo liachwe ili alifikishe kwa Waziri Mkuu kwa hatua zaidi. Hata hi