Inauma Jamani..Hii Hapa Simulizi ya Mtoto wa D' Banj Aliyefariki Kwa Kudumbukia Kwenye Swimming Pool
STAA wa Muziki wa Afrobeats, Oladapo Daniel Oyebanjo ‘D’Banj’ na mkewe Didi Lineo, wamepoteza mtoto wao wa kiume aitwaye Daniel, aliyekuwa na umri wa mwaka na miezi mitatu aliyefia kwenye bwawa la kuogelea.
Daniel alifariki siku ya Jumapili mchana, katika nyumba ya staa huyo aliyewahi kutamba na Wimbo wa Oliver Twist, huko Ikoyi, Lagos, Nigeria wakati akiwa anacheza bwawani.
ILIKUWAJE?
Taarifa za ndani kutoka kwenye familia ya D’Banj, zinaeleza kuwa katika mchana huo Daniel alikuwa akicheza na watoto waliotembelea nyumbani hapo, ambao baadaye walimuacha peke yake na ndipo alipodumbukia kwenye bwawa.
Mwili wake ulikutwa kwenye bwawa hilo baadaye na mama yake aliyefikiri alimuacha na watoto wakubwa ambao wangemjali, baada ya kumuona mwanaye akiwa bwawani mara moja alimchukua na kumkimbiza hospitali lakini aliambiwa kwamba alikwishafariki na kupelekwa mochwari.
D’ BANJ ALIKUWA WAPI?
Wakati mtoto wake huyo wa kwanza akifariki, D’Banj hakuwepo Lagos, siku moja kabla (Jumamosi), alikuwa ameruka kwa ndege kwenda Los Angeles, kuhudhuria Tuzo za BET, zilizotolewa usiku wa Jumapili.
Hata hivyo kutokana na kifo hicho, D’ Banj hakufanikiwa kuhudhuria Tuzo za BET. Ilibidi arudi mara moja Nigeria huku akimuacha staa mwenzake kutoka Nigeria, Davido ambaye usiku huo alipata Tuzo ya Msanii Bora Kutoka Nje ya Marekani.
D’ Banj pia aliposti picha ya ‘background’ nyeusi kwenye Mtandao wa Instagram na kuandika hivi; “Ni muda wa majaribu… lakini Mungu wangu siku zote daima ni mwaminifu.”
MASTAA WAMPA POLE
Kwa upande wa Davido, wakati akipokea tuzo yake kabla ya kushu-kuru alisema kwamba; “Kabla sijaen-delea naomba kutuma salamu za pole kwa kaka yangu, ambaye alipambana kutengeneza hii njia ambayo kila msanii Afrika leo anaifurahia kwa kupoteza mtoto wake wa kiume.”
Lakini pia mastaa mbalimbali duniani akiwemo Banky W, walimpa pole staa huyo ambaye yupo kwenye Lebo ya Kanye West ya G.O.O.D Music.
Comments
Post a Comment