Posts

Showing posts from June 20, 2018

Hamisa Mobetto Atoa Mpya 'Kuna Muda Natamani Kuondoka Tanzania ila....."

Image
Muigizaji wa Bongo movie na mzazi mwenza wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Hamisa Mobetto amedai kuwa kuna muda anatamani kuondoka Tanzania. Hamisa ambaye ameendelea kushika headlines kwani tangu alivyotangaza kuwa ana ujauzito wa Diamond mwaka jana basi hajatoka midomoni kwa watu tena. Hamisa siku ya jana alizuahgumzo baada ya kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa anatamani kuondoka Tanzania lakini kila akifika airport anajuuliza Watanzania wataishije bila yeye. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Hamisa aliandika: Sometimes, Natamani Kuondoka Tanzania nafika hadi airport ila najiuliza Watanzania Wenzangu Wataishije Bila Mimi“. Hamisa amekuwa akiongelewa sana Kwenye mitandao ya kijamii siku hizi tangu arudiane na Diamond na kiukweli imekuwa burudani kwa mashabiki zao hasa ukimuweka Diamond huku Zari pale na Hamisa huku.

Chazi Baba Amwagana na Mkewe Kisa Hiki Hapa

Image
UBUYU siku zote hauhitaji kijiwe maalumu cha kuumung’unya popote unaumung’unya tu iwe barabarani, kiwanjani hata kwenye gari twende tu! Mwanamuziki ambaye alikuwa memba wa bendi maarufu ya Mashujaa, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’, amedaiwa kumwagana na mke wake wa ndoa Rehema Sospeter kutokana na ugomvi wa mara kwa mara. Msambaza ubuyu huu mtamu kutoka Zenji, alisema kuwa mara nyingi kumekuwa kukitokea ugomvi kati ya mwanamuziki huyo na mkewe kiasi ambacho kwa hivi sasa imebidi kila mtu kuangalia ustaarabu wake na kwamba kuna tetesi za ukweli kuwa mwanamuziki huyo karudisha mapenzi kwa mzazi mwenzake Husna Idd ‘Sajenti’. “Unajua Chaz na mkewe huyo mara nyingi wamekuwa wakigombana mara kwa mara kisha wanawekwa sawa wanarudiana tena. Lakini safari hii inaonekana wazi kuwa ndoa yao haipo tena, kwani mwanamke huyo kabeba kila kitu ndani kaondoka na ni muda mrefu sasa hawaishi pamoja na mwanamuziki huyo amerudisha mapenzi kwa Sajenti,” kilisema chanzo hicho. TUMCHEKI KWANZA SAJENTI I

Mwenyekiti wa CHADEMA ashambuliwa

Image
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwikatsi wilayani Babati mkoani Manyara, Simon Lala (CHADEMA) ameshambuliwa na watu wasiojulikana waliomjeruhi kwa mishale na mapanga kwa kile kilichodaiwa kuwa ni mgogoro wa ardhi. Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Agustino Senga ameiambia eatv.tv kuwa shambulio hilo limetokea Juni 18, 2018 katika kitongoji cha Waloa wakati mwenyekiti huyo kwa tiketi ya CHADEMA akiwa kazini pamoja na wajumbe wa serikali ya kijiji. Kamanda Senga amesema kuwa mwenyekiti huyo ameshambuliwa akitekeleza majukumu yake ambapo alikuwa akisimamia kesi ya ndugu wakigombea ardhi na ndipo upande wa walioshindwa hawakuridhishwa na matokeo ya baraza la kata. “Tukio lilitokea mida ya saa 5:00 asubuhi wakati mwenyekiti akiwa shambani akimuonesha mipaka ndugu wa watuhumiwa hao waliokimbia baada ya kutekeleza shambulio hilo, ambao walishindwa katika kesi ya kugombea ardhi lakini hawakuridhishwa na matokeo na kudai mwenyekiti kafanya upendeleo”, ames

Maskini..Kaka wa Eric Omondi afariki dunia Kwa Madawa ya Kulevya..Asimulia Walivyohangaika Nae

Image
Taarifa zilizotufikia leo June 19,2018 ni kuhusu kifo cha kaka mkubwa wa mchekeshaji maarufu nchini Kenya Eric Omondi ambaye amefariki asubuhi ya kuamkia leo na kifo chake kimesababishwa na matumizi ya dawa za kulevya. Kupitia ukurasa wa Instagram wa Eric Omondi ameelezea kuhusiana na kifo cha kaka yake Joseph Onyango Omondi ikiwa ni saa 12 baada ya kupatikana mtaa wa Downton River Nairobi na kukubali kumsaidia kurudi katika hali yake ya kawaida na kuachana na dawa za kulevya.  “Hii sio picha ya mwisho ya kaka yangu niliotaka kuipost, lakini ni picha ambayo nataka kila kijana kwenye hii nchi kuiona. Joseph Onyango Omondi amefariki leo asubuhi saa tisa, ikiwa ni saa 12  baada ya kumkuta Downton River Road “ “Alikuwa akitumia dawa za kulevya aina ya Cocaine na vitu vingine na alikuwa akienda Rehab na kutoka kwa Milka 19, Mungu mwenyewe ndio atatoa malipo. Namshukuru kila mmoja ambaye alikuja jana kutusaidia”

Wema Sepetu Sasa Kupumua Tarehe 16 July Kujulikana Mbifu na Mbichi

Image
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Msanii Wema Sepetu na wafanyakazi wake wawili July 16,2018. Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya mawakili wa upande wa utetezi kufunga ushahidi wao wa mashahidi watatu akiwemo Wema. Mbali ya Wema, katika kesi hiyo washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abas. Hakimu Simba amesema mahakama hiyo inatarajia kutoa hukumu hiyo July 16,2018 baada ya kufungwa kwa ushahidi wa utetezi uliokuwa na mashahidi 3 akiwemo Wema. Awali kabla ya kupangwa kwa tarehe ya hukumu Wema na wafanyakazi wake walijitetea, ambapo Wema amedai kuwa ni kweli nyumbani kwake kulikutwa msokoto unaodhaniwa kuwa ni bangi na vipisi. Katika hoja zake, Wema amedai kuwa hajui vitu hivyo ni vya nani kwa sababu yeye ni msanii wa Filamu na nyumbani kwake wanaingia watu tofauti tofauti pia huwa anafanya Party na kualika watu katika nyama choma na chakula cha mch

Kagera Sugar Yashindwana na Kaseja Yamruhusu Kwenda Popote

Image
NI kama uongozi wa Kagera Sugar umeamua kumruhusu mlinda mlango wao mahiri, Juma Kaseja, kujiunga na timu yoyote ambako ataona yeye kunamfaa baada ya kushindwana na uongozi wa timu hiyo. Kaseja ambaye alishawahi kuzitumikia klabu za Simba na Yanga kabla ya kujiunga na Mbeya City na kisha kujiunga na Kagera Sugar ameshaelezwa kuwa anaweza kuondoka hapo. Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Kagera Sugar, Mohamed Hussein, alisema kuwa walikaa kikao jana kujadili juu ya kuongeza wachezaji wapya katika timu yao baada ya kocha wao kuwasilisha ripoti yake juzi. “Mwalimu alitupatia ripoti Jumapili baada ya kumaliza sikukuu ya Eid na Jumatatu tulikaa kikao na viongozi wengine na yeye kocha (Mecky Mexime), nadhani hatutasajili wachezaji wengi ila tutaangalia wachezaji ambao wataondoka, lazima tuangalie wachezaji mbadala. “Juma Kaseja tupo naye kwenye mazungumzo, lakini kama atapata timu ya kwenda, tunamruhusu kwenda. “Sisi tunaamini kuna wachezaji wengi wenye kipaji kama Kaseja,

Irene Uwoya Aachia Picha za Utata Mtandaoni na Kusema Haya..

Image
Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya na mke halali wa mwanamuziki Dogo Janja amewatolea uvivu mashabiki zake kwenye mtandaoo wa kijamii kuwa sio wa kwanza yeye kuvaa nguo za ufukweni hivyo wasimpangie chakufanya kwa madai vazi hilo mume wake amelipenda nasio vinginevyo. Uwoya ametoa kauli hiyo asubuhi ya leo kupitia mtandao wake wa kijamii baada ya kupita siku moja tokea alipo-post picha aliyokuwa amevalia vazi jeupe lililokuwa linaonesha maumbile yake ya mwili na kusababisha mashabiki zake kumtolea maneno makali kuwa haeshimu ndoa yake wala mume wake kwa kuwa anachokifanya sasa hakipendezi na wadhfa wake aliokuwa nao. "Ukivaa nguo kawaida ana kigodoro, nikim-post mume oonh mdogo na nisipo post kwanini hum-post mara humpendi. Nikivaa nguo za ufukweni nipo uchi mke wa mtu, sasa nasema hivi kwa wale iliyowauma poleni sana siku nyingine ntawashirikisha nikitaka ku-post. Hivi kwani mimi ni wa kwanza bongo kuvaa hivi maeneo ya ufukweni. Mume wangu kaipenda balaah yani", ameand