Nuh Mziwanda Apiga Moyo Konde 'Sinta Futa Tattoo ya Shilole Mwilini Kwangu'


Msanii wa kizazi kipya bongo, Nuh Mziwanda ameweka wazi sababu zinazomfanya mpaka leo hajafuta Tatoo za waliowahi kuwa wapenzi wake ni kwasababu alizichora akiwa na mapenzi na bado zina maana kubwa sana katika maisha yao.

Mziwanda ameyaanika hayo leo alipokuwa kwenye kipindi cha DADAZ, kinachorushwa kila Jumatano kupitia EATV ambapo msanii huyo amesema kuwa wakati anachora Tatoo ya msanii Shilole aliyewahi kuwa mpenzi wake alifanya kwa moyo na hakulazimishwa.

Akizungumzia tatoo hizo, Nuh amesema kuwa licha ya kuwa yeye ni mpenzi wa tattoo lakini pia Shilole ni mwanamke alimfunza mambo mengi ya kimaisha hasa alipochukua majukumu ya kuishi naye kama mume na mke wakati yeye akiwa na umri mdogo  kuliko mwenzake.

"Mimi napenda sana 'Tatoo' na zote nilizochora  huwa zinamaana. Lakini pia sijawahi kufuta, hata niliyomchora Shilole. Sijaiacha 'Tatoo' ya Shilole katika mwili wangu kwa sababu bado nampenda, hapana. Lakini nimeiacha kwa sababu ni mwanamke ambaye alinifunza mambo mengi sana hasa maisha wakati naishi naye, " - Msanii Nuh Mziwanda.
Nuh ambaye hana tatoo moja ya mwanamke katika mwili wake amesema kwamba, tatoo ya Nawal, katika mwili wake bado ina maana kubwa kwa kuwa ni mwanamke ambaye amemzalia mtoto wake.

Pamoja na hayo msanii huyo ameweka wazi hafikirii kuzifuta tatoo hizo hata kama wanawake hao walishafuta zile walizomchora, ambapo amesema kuwa hiyo inatokana kwamba walichora kwa kufuata mkumbo  au labda walifanya bila kutoka moyoni.
"Nipo kwenye mahusiano na mwanamke mwingine, hapendi hizi tatoo lakini nimeshamuelewesha na ameelewa ingawa anakasirika akiiona" Nuh.

Comments

Popular posts from this blog

Diamond aibua jipya tuhuma za Hamisa Mobetto kupigwa na Bi. Sandrah

Idris Sultan ‘Mi Nina Kiingereza, Shilole una Nyumba Nani Anamcheka Mwenzie’

Sababu ya kuachiwa Babu Tale ni kuwa amri ya kumkamata yeye na ndugu yake Idd Shaban Taletale ilitolewa kimakosa

Zari Amkumbuka Ivan Katika Kumbukumbu Ya Kifo Chake....Leo Katimiza Mwaka Mmoja

Diamond Platnumz Apewa Gari Mpya na Uongozi wake wa Wasafi