Chazi Baba Amwagana na Mkewe Kisa Hiki Hapa

UBUYU siku zote hauhitaji kijiwe maalumu cha kuumung’unya popote unaumung’unya tu iwe barabarani, kiwanjani hata kwenye gari twende tu! Mwanamuziki ambaye alikuwa memba wa bendi maarufu ya Mashujaa, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’, amedaiwa kumwagana na mke wake wa ndoa Rehema Sospeter kutokana na ugomvi wa mara kwa mara.

Msambaza ubuyu huu mtamu kutoka Zenji, alisema kuwa mara nyingi kumekuwa kukitokea ugomvi kati ya mwanamuziki huyo na mkewe kiasi ambacho kwa hivi sasa imebidi kila mtu kuangalia ustaarabu wake na kwamba kuna tetesi za ukweli kuwa mwanamuziki huyo karudisha mapenzi kwa mzazi mwenzake Husna Idd ‘Sajenti’.

“Unajua Chaz na mkewe huyo mara nyingi wamekuwa wakigombana mara kwa mara kisha wanawekwa sawa wanarudiana tena. Lakini safari hii inaonekana wazi kuwa ndoa yao haipo tena, kwani mwanamke huyo kabeba kila kitu ndani kaondoka na ni muda mrefu sasa hawaishi pamoja na mwanamuziki huyo amerudisha mapenzi kwa Sajenti,” kilisema chanzo hicho.

TUMCHEKI KWANZA SAJENTI

Ijumaa Wikienda: Mambo vipi Sajenti? Nasikia sasa hivi wewe na mzazi mwenzio mmerudiana?

Sajenti: Mzazi mwenzangu nani kwanza unamzungumzia?

Ijumaa Wikienda: Kwani humjui baba wa mtoto wako wa kwanza si Chaz Baba?

Sajenti: Sasa hapo unataka mimi nijibuje au ulienda nyumbani kwake ukatukuta tupo wote?

Ijumaa Wikienda: Ndio maana nimekupigia nikijua wazi utanipa ukweli wa jambo hilo?

Sajenti: Sina ukweli (akakata simu).


CHAZ BABA AFUNGUKA

Baada ya kuzungumza na Sajenti gazeti hili lilimtafuta Chaz Baba, ambaye alisema kuwa kwa sasa yupo mkoani Tabora kuna bendi mpya iitwayo Smart anapiga mzigo na alipoulizwa madai hayo ya kumwagana na mkewe na kurudisha mapenzi kwa Sajenti alifunguka kama ifuatavyo:

Ijumaa Wikienda: Chaz habari za siku nyingi? Vipi mkeo hajambo?

Chaz Baba: Atakuwa hajambo.

Ijumaa Wikienda: Kwa nini atakuwa hajambo kwani hamuishi naye nyumba moja?

Chaz Baba: Kwa sasa tuna matatizo kidogo hivyo karudi kwao.

Ijumaa Wikienda: Kwa hiyo sasa hivi ndio unaishi na Sajenti?

Chaz Baba: Hapana naishije naye sasa wala siwezi kurudiana naye, yule ni mzazi mwezangu na itabaki kuwa hivyo na si vinginevyo na kama watu walituona mahali itakuwa ni kwa ajili ya mtoto wetu tu.

Ijumaa Wikienda: Vipi sasa kuhusu wewe na mkeo ndio moja kwa moja? Hatorudi kwako tena?

Chaz Baba: Unajua mimi nilioa mke mmoja na siwezi kuoa tena hivyo nina imani hayo tutayamaliza kifamilia na atarudi nyumbani na tutaendelea na maisha kama kawaida.

Ijumaa Wikienda: Mbona kuna tetesi kabeba kila kitu chake?

Chaz Baba: Kwani kubeba kila kitu kutamfanya asirudi kwake? Si atarudi tena na hivyo vitu.
Chanzo: Global Publishers

Comments

Popular posts from this blog

Diamond aibua jipya tuhuma za Hamisa Mobetto kupigwa na Bi. Sandrah

Idris Sultan ‘Mi Nina Kiingereza, Shilole una Nyumba Nani Anamcheka Mwenzie’

Sababu ya kuachiwa Babu Tale ni kuwa amri ya kumkamata yeye na ndugu yake Idd Shaban Taletale ilitolewa kimakosa

Zari Amkumbuka Ivan Katika Kumbukumbu Ya Kifo Chake....Leo Katimiza Mwaka Mmoja

Diamond Platnumz Apewa Gari Mpya na Uongozi wake wa Wasafi