Wema Sepetu Sasa Kupumua Tarehe 16 July Kujulikana Mbifu na Mbichi

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu inatarajia kutoa hukumu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili Msanii Wema Sepetu na wafanyakazi wake wawili July 16,2018.

Hukumu hiyo inatarajiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya mawakili wa upande wa utetezi kufunga ushahidi wao wa mashahidi watatu akiwemo Wema.

Mbali ya Wema, katika kesi hiyo washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abas.

Hakimu Simba amesema mahakama hiyo inatarajia kutoa hukumu hiyo July 16,2018 baada ya kufungwa kwa ushahidi wa utetezi uliokuwa na mashahidi 3 akiwemo Wema.

Awali kabla ya kupangwa kwa tarehe ya hukumu Wema na wafanyakazi wake walijitetea, ambapo Wema amedai kuwa ni kweli nyumbani kwake kulikutwa msokoto unaodhaniwa kuwa ni bangi na vipisi.

Katika hoja zake, Wema amedai kuwa hajui vitu hivyo ni vya nani kwa sababu yeye ni msanii wa Filamu na nyumbani kwake wanaingia watu tofauti tofauti pia huwa anafanya Party na kualika watu katika nyama choma na chakula cha mchana.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kutumia dawa za kulevya.

Inadaiwa kuwa Februari4,2017 katika Makazi ya Wema huko Kunduchi Ununio washtakiwa hao walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito wa gramu 1.08.

Comments

Popular posts from this blog

Diamond aibua jipya tuhuma za Hamisa Mobetto kupigwa na Bi. Sandrah

Idris Sultan ‘Mi Nina Kiingereza, Shilole una Nyumba Nani Anamcheka Mwenzie’

Sababu ya kuachiwa Babu Tale ni kuwa amri ya kumkamata yeye na ndugu yake Idd Shaban Taletale ilitolewa kimakosa

Zari Amkumbuka Ivan Katika Kumbukumbu Ya Kifo Chake....Leo Katimiza Mwaka Mmoja

Diamond Platnumz Apewa Gari Mpya na Uongozi wake wa Wasafi