Mwenyekiti wa CHADEMA ashambuliwa

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwikatsi wilayani Babati mkoani Manyara, Simon Lala (CHADEMA) ameshambuliwa na watu wasiojulikana waliomjeruhi kwa mishale na mapanga kwa kile kilichodaiwa kuwa ni mgogoro wa ardhi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Agustino Senga ameiambia eatv.tv kuwa shambulio hilo limetokea Juni 18, 2018 katika kitongoji cha Waloa wakati mwenyekiti huyo kwa tiketi ya CHADEMA akiwa kazini pamoja na wajumbe wa serikali ya kijiji.

Kamanda Senga amesema kuwa mwenyekiti huyo ameshambuliwa akitekeleza majukumu yake ambapo alikuwa akisimamia kesi ya ndugu wakigombea ardhi na ndipo upande wa walioshindwa hawakuridhishwa na matokeo ya baraza la kata.

“Tukio lilitokea mida ya saa 5:00 asubuhi wakati mwenyekiti akiwa shambani akimuonesha mipaka ndugu wa watuhumiwa hao waliokimbia baada ya kutekeleza shambulio hilo, ambao walishindwa katika kesi ya kugombea ardhi lakini hawakuridhishwa na matokeo na kudai mwenyekiti kafanya upendeleo”, amesema Kamanda.

Kwa upande wake Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Kilimanjaro, Basil Lema amesema mwenyekiti huyo atahamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC kwa matibabu zaidi baada ya kupewa rufaa katika Hospital ya Mkoa wa Manyara.

Comments

Popular posts from this blog

Diamond aibua jipya tuhuma za Hamisa Mobetto kupigwa na Bi. Sandrah

Idris Sultan ‘Mi Nina Kiingereza, Shilole una Nyumba Nani Anamcheka Mwenzie’

Sababu ya kuachiwa Babu Tale ni kuwa amri ya kumkamata yeye na ndugu yake Idd Shaban Taletale ilitolewa kimakosa

Zari Amkumbuka Ivan Katika Kumbukumbu Ya Kifo Chake....Leo Katimiza Mwaka Mmoja

Diamond Platnumz Apewa Gari Mpya na Uongozi wake wa Wasafi