Irene Uwoya Aachia Picha za Utata Mtandaoni na Kusema Haya..


Msanii wa filamu nchini Irene Uwoya na mke halali wa mwanamuziki Dogo Janja amewatolea uvivu mashabiki zake kwenye mtandaoo wa kijamii kuwa sio wa kwanza yeye kuvaa nguo za ufukweni hivyo wasimpangie chakufanya kwa madai vazi hilo mume wake amelipenda nasio vinginevyo.

Uwoya ametoa kauli hiyo asubuhi ya leo kupitia mtandao wake wa kijamii baada ya kupita siku moja tokea alipo-post picha aliyokuwa amevalia vazi jeupe lililokuwa linaonesha maumbile yake ya mwili na kusababisha mashabiki zake kumtolea maneno makali kuwa haeshimu ndoa yake wala mume wake kwa kuwa anachokifanya sasa hakipendezi na wadhfa wake aliokuwa nao.
"Ukivaa nguo kawaida ana kigodoro, nikim-post mume oonh mdogo na nisipo post kwanini hum-post mara humpendi. Nikivaa nguo za ufukweni nipo uchi mke wa mtu, sasa nasema hivi kwa wale iliyowauma poleni sana siku nyingine ntawashirikisha nikitaka ku-post. Hivi kwani mimi ni wa kwanza bongo kuvaa hivi maeneo ya ufukweni. Mume wangu kaipenda balaah yani", ameandika Uwoya.
Kwa tamaduni za kiafrika na kitanzania mara zote watu wanaamini endapo mwanamke atakapokuwa ameolewa basi kuna mavazi huwa anaepuka kuyavaa hata kama akiwa kwenye fukwe za bahari na hicho ndicho mashabiki zake walichokiamini lakini kwa bahati mbaya leo wamekutana na jambo la utofauti.

Comments

Popular posts from this blog

Diamond aibua jipya tuhuma za Hamisa Mobetto kupigwa na Bi. Sandrah

Idris Sultan ‘Mi Nina Kiingereza, Shilole una Nyumba Nani Anamcheka Mwenzie’

Sababu ya kuachiwa Babu Tale ni kuwa amri ya kumkamata yeye na ndugu yake Idd Shaban Taletale ilitolewa kimakosa

Zari Amkumbuka Ivan Katika Kumbukumbu Ya Kifo Chake....Leo Katimiza Mwaka Mmoja

Diamond Platnumz Apewa Gari Mpya na Uongozi wake wa Wasafi