Nuh Mziwanda Azungumzia Picha Zake Tata na Amber Lulu
Msanii wa muziki wa bongo fleva Nuh Mziwanda amaefunguka na kuzungumzia video tata iliyokuwa ikiwaonyesha yeye na msanii mwenzake wa kike Amber lulu wakiwa sehemu faragha wakiwa katika mapozi ya kimahaba.
Wawili hao wanasadikika kuwa wapenzi hasa baada ya kuonekana kwa vido hiyo ambayo ilisambaa kupitia snap chat ya Amber Lulu.
Kwa mujibu wa Nuh anasema kuwa hakuna chochote kinachoendelaa kimapenzi kati yao bali kuna project wameeianda kati yao na ile iliyovuja walikuwa location kwa ajili ya ku-shoot.
"Mimi na Amber tuna project na hakuna kitu chochote, ila mimi niko snap chat kwaio wakati tunashoot video kulikuwa na zile vibes za snapchat za kucheka, ku-enjoy na kufanya mambo mengine mengi , yeye alikuwa akichukua kwenye sanap na mimi nilikuwa nachukua katika snap lakini haikuwa kwa ubaya, na wala sikumwambia aitoe maana pale ile ni snapchat yake."
Comments
Post a Comment