MSAMI “Nilivyoachana na Uwoya Nilikuwa Bado Nampenda”
Jana May 30, 2018 kupitia kipindi cha XXL cha Clouds Fm dancer na pia msanii wa Bongofleva Msami alifanya mahojiano na kuongea vitu kibao ikiwemo mahusiano yake na muigizaji Irene Uwoya ambaye kwa sasa ni mke halali wa Dogo Janja.
Msami amefunguka na kusema kuwa Godzilla aliwahi kumpigia simu aliyekuwa mpenzi wake Irene Uwoya na kumzungumzia vibaya juu yake na hakujua lengo halisi la Godzilla kufanya hivyo ilikuwa ni nini hasa.
“Wakati nikiwa na mahusiano na Irene Uwoya Godzilla alimpigia simu uwoya na kunipondea sana”
Msami ameongezea pia na kusema kuwa wakati anaachana na Irene Uwoya alikuwa bado anampenda.
Comments
Post a Comment