Tangu wiki iliyopita zimesambaa taarifa za Hamisa Mobetto kuchezea kipigo cha ‘Mbwa Koko’ kutoka kwa mama yake Diamond – Hata hivyo ukweli wa taarifa hizo haukuwezekana kufahamika mpaka sasa. Lakini Diamond ameonekana kuibua upya suala hilo huku akionekana kutoa jibu la tukio hilo lakini kwa kutumia njia ya mafumbo. Msanii huyo wa WCB, amecomment kwenye video ya mama yake ambayo ameiweka kwenye mtandao wa Instagram kwa kumfananisha mama huyo na bondia aliyekuwa hatari zaidi ulingoni, Mike Tyson.
Mchekeshaji Idris Sultan amezua hii jingine kupitia ukuarasa wake wa instagram baada ya kum-post Shilole “Shishi baby” na kuandika caption ambayo imezua gumzo kwa mashabiki kutokana na comments zilizoandikwa kupitia picha hiyo. Idris Sultan aliandika “Ana nyumba, ana bishara zaidi ya tatu, ana watoto, ameolewa na ni maarufu na bado ana baby face. Mi nina kiingereza tu. Tuendelee kuendekeza ujinga tutajua nani anamcheka mwenzake 😂🙌🏽”
Sababu za kuachiwa Hamis Shaban Taletale maarufu kama Babu Tale mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Tip Top Connection, aliyekuwa akisota mahabusu, akisubiri amri ya kupelekwa kifungoni gerezani, zimebainika. Babu Tale ambaye pia ni meneja wa mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul, ‘Diamond Platnumz’, aliachiwa kwa muda na Jaji Edson Mkasimongwa, kwa kile kilichoelezwa kuwa amri ya kumkamata yeye na ndugu yake Idd Shaban Taletale ilitolewa kimakosa. Kwa mujibu wa chanzo chetu kutoka mahakamani hapo, makosa yaliyobainika katika amri hiyo ni kwamba aliyeitoa, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Dar es Salaam, Wilbard Mashauri hakuwa na mamlaka ya kutoa amri hiyo na kwamba ilikuwa haieleweki. Hivyo Jaji Mkasimongwa alimwachia jana kwa muda lakini akamtaka afike mahakamani saa 6:00 mchana, leo Mei 25, 2018. Babu Tale alitiwa mbaroni Jumanne Mei 22, 2010, kwa amri ya mahakama hiyo iliyotolewa na Naibu Msajili Mashauri Februari 16 na hati ya kuwakamata iliyotolewa
Zarinah Hassan maarufu kama Zari The Bosslady amezidi kumkumbuka aliyekuwa mume wake Ivan Semwanga aliyeaga dunia mwaka jana tarehe 25 mwezi wa tano. Ivan ametimiza mwaka mmoja Tangu alipofariki mwaka jana nchini Afrika ya Kusini kutokana na maradhi ya moyo. Zari alijaliwa kupata watoto watatu wa kiume na marehemu Ivan na walikuwa katika Mahusiano kwa miaka mingi sana. Zari alianza kumuenzi Marehemu Ivan tangu jana ambapo aliandika ujumbe huu Kwenye ukurasa wake wa Instagram:
Msanii wa Bongo Fleva Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz amekabidhiwa ndinga mpya ya kifahari na uongozi wake wa WCB. Muimbaji huyo mapema leo alipost video fupi akionyesha gari hiyo ya kisasa aina ya Toyota Land Cruiser. “Management yangu imenipatia Toy hii ndogo kwa ajili ya mikutano yangu ya kampuni,” alindika Diamond kupitia Instagram
Comments
Post a Comment