“Sijaongea na familia ya Masogange” - Belle 9

Msanii wa muziki nchini Abelnego Damian, maarufu kama Belle 9, amesema kuwa bado hajaongea na familia ya msanii marehemu Agnes Gerard “Masogange” kuhusu kumsaidia mtoto wa marehemu kwasababu hakuwa na ukaribu na familia hiyo.

Belle 9 amesema hayo jana Mei 25, 2018 katika kipindi cha FRIDAY NIGHT LIVE kinachorushwa na EATV kila siku ya Ijumaa saa 3:00 usiku na kuongeza kuwa aliifahamu familia ya Agnes Gerard “Masogange” baada ya kutokea msiba hivyo imekuwa ngumu kwa yeye kuwasiliana nao.

“Sijapata nafasi ya kuongea chochote kwasababu hatukua karibu sana na pia hakuna mtu alitarajia, kwahiyo sijaongea chochote kuhusiana na mambo ya familia kwamba nitafanya chochote kuhusu yule mtoto” amesema Belle 9

Belle 9 ameongeza kuwa alihuzunika sana kutokana na kifo cha msanii huyo kwasababu ya ukaribu waliokuwa nao, pia “Masogange” alichangia kwa kiasi kikubwa katika mafanikio yake ya muziki baada ya  kushiriki katika video ya wimbo wake wa “Masogange”.

Marehemu Agnes Gerard alipata umaarufu baada ya kushiriki  katika video ya wimbo wa msanii Belle 9 ulioitwa “Masogange” mwaka 2009.

April 20, 2018 Agnes Gerard “Masogange” alifariki Dunia Jijini Dar es salaam baada ya kuzidiwa na homa ya tumbo na upungufu wa damu na alizikwa nyumbani kwao Utengule-Mbalizi Mkoani Mbeya April 23, 2018.

Comments

Popular posts from this blog

Diamond aibua jipya tuhuma za Hamisa Mobetto kupigwa na Bi. Sandrah

Idris Sultan ‘Mi Nina Kiingereza, Shilole una Nyumba Nani Anamcheka Mwenzie’

Sababu ya kuachiwa Babu Tale ni kuwa amri ya kumkamata yeye na ndugu yake Idd Shaban Taletale ilitolewa kimakosa

Zari Amkumbuka Ivan Katika Kumbukumbu Ya Kifo Chake....Leo Katimiza Mwaka Mmoja

Diamond Platnumz Apewa Gari Mpya na Uongozi wake wa Wasafi