Ofisi ya Mbunge Ridhiwani Kikwete ilivyoungua Moto Jana, Mwanamke Kichaa Atajwa Kusababisha Moto

Ofisi ya Mbunge jimbo la Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete iliyopo eneo la Msolwa, Chalinze imeungua kwa moto jioni hii ya leo Jumapili, Juni 17, 2018 huku mali, samani na nyaraka zilizokuwemo ndani ya jengo hilo zikitejetea vibaya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi Jonathan Shana amethibitisha na kusema chanzo cha moto huo ni mwanamke anayedaiwa kuwa ana matatizo ya akili ‘kichaa’ alikuwa na moto nje ya ofisi, upepo ulipopiga ulisukuma moto ukashika jengo.

Global Publishers imefika eneo la tukio na kushuhudia moto huo ukiteketeza jengo hilo na vitu vilivyokuwemo huku ukitambaa na kuelekea kwenye nyasi zilizo jilani na jengo,

Aidha, Kikosi cha zimamoto kilifika eneo la tukio lakini tayari moto ulikuwa umeshashika jengio zima hivyo hakuna dalili za kuokoa chochote.

Comments

Popular posts from this blog

Diamond aibua jipya tuhuma za Hamisa Mobetto kupigwa na Bi. Sandrah

Idris Sultan ‘Mi Nina Kiingereza, Shilole una Nyumba Nani Anamcheka Mwenzie’

Sababu ya kuachiwa Babu Tale ni kuwa amri ya kumkamata yeye na ndugu yake Idd Shaban Taletale ilitolewa kimakosa

Zari Amkumbuka Ivan Katika Kumbukumbu Ya Kifo Chake....Leo Katimiza Mwaka Mmoja

Diamond Platnumz Apewa Gari Mpya na Uongozi wake wa Wasafi