Malalamiko ya TID ‘yamfikia’ Professor Jay, Alichojibu

Msanii wa muziki wa hip hop Bongo, Professor Jay amejibu kile alichodai TID kuwa wasanii wengi wa zamani wamezulumiwa fedha nyingi na sasa ambao ni wakati wao wa kula matunda wanawekwa pembeni kwa kuelezwa kuwa ni wakongwe.

Sasa Professor Jay amesema hilo linatokana na wasanii kutofanya kazi kwa uweledi wa kisheria na wasanii wengi wa mwanzo katika Bongo Flava walikuwa wakifanya kazi kirafiki zaidi.

“Kujiongeza, tuwe professional, ukiwa professional maana kuna wanasheria, kuna mameneja, unaweza ukawa na meneja hata mameneja wengi sasa hivi ni washikaji zetu. Tatizo kubwa tulilokuwa tunafanya tulikuwa tunafanya kazi sana kirafiki,” Professor Jay ameiambia Clouds TV.

Soma Pia; Diamond naye wanataka kumuua, sijui wanataka kumuweka nani – TID

Hivi karibuni TID alitoa lawama zake kwa media ambazo hakuzitaja kuwa zimekuwa na mtindo wa kuwashusha wasanii pindi wanapodai maslai yao na kuwaeleza wakati wao umepita na kuwapandisha wengine.

“Ni kukutoa kwenye line ili kuwaweka watu wao, kwa vile sisi tunawadai wametuzulumu sana. Na kweli anaweza because he has a media,” alisema TID.

Comments

Popular posts from this blog

Diamond aibua jipya tuhuma za Hamisa Mobetto kupigwa na Bi. Sandrah

Idris Sultan ‘Mi Nina Kiingereza, Shilole una Nyumba Nani Anamcheka Mwenzie’

Sababu ya kuachiwa Babu Tale ni kuwa amri ya kumkamata yeye na ndugu yake Idd Shaban Taletale ilitolewa kimakosa

Zari Amkumbuka Ivan Katika Kumbukumbu Ya Kifo Chake....Leo Katimiza Mwaka Mmoja

Diamond Platnumz Apewa Gari Mpya na Uongozi wake wa Wasafi