Dully ni 'Mshenzi' - Master J

NA FATUMA MUNA
Mtayarishaji mkongwe wa muziki wa Bongo fleva, Joachim Kimario ‘Master J’ amefunguka na kumshukuru Msanii Dully Sykes kwa kuufanya wimbo wa Dhahabu kuwa mkubwa ingawa ni 'mshenzi'.

Master Jay ameyasema hayo akiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa, wakati akisimulia namna ambavyo wimbo wa 'dhahabu' uliofanywa na Dully akiwa amemshirikisha Joseline na Mr. Blue ulivyorekodiwa.

"Wakati wa natengeneza wimbo wa 'Dhahabu' Dully alinitesa sana siku hiyo. Kwanza alikuja studio na totoz mbili alafu ananukia mno nikampa beat aifanyie kazi, Duly wewe ni mshenzi sana. Alirekodi wimbo mzima mic ikiwa imegeuka nyuma, alipomaliza akanambia Master hiyo itakutosha halafu akaondoka zake na totoz zake," Master J

Ameongeza kwamba "Nilihangaika sana mpaka hizo sauti mnazisikia hivo. Namshukuru Mungu, Mungu mkubwa wimbo ulikuja kuwa mkubwa. Huyo ndiyo misifa, Namshukuru alinipatia 'hit song"

Mbali na hayo Master Jay amesema kwa sasahivi wasanii wanashindwa kutengeneza nyimbo kali kutokana na watu wengi hawaangalii vipaji.

Comments

Popular posts from this blog

Diamond aibua jipya tuhuma za Hamisa Mobetto kupigwa na Bi. Sandrah

Idris Sultan ‘Mi Nina Kiingereza, Shilole una Nyumba Nani Anamcheka Mwenzie’

Sababu ya kuachiwa Babu Tale ni kuwa amri ya kumkamata yeye na ndugu yake Idd Shaban Taletale ilitolewa kimakosa

Zari Amkumbuka Ivan Katika Kumbukumbu Ya Kifo Chake....Leo Katimiza Mwaka Mmoja

Diamond Platnumz Apewa Gari Mpya na Uongozi wake wa Wasafi