Trump anafikiria kuongeza umri wa kununua silaha Marekani
Bunduki aina ya AR-15
Rais wa Marekani Donald Trump ameidhinisha wazo la kuwaruhusu waalimu kubeba silaha ndani ya darasa. Rais Trump alisema hayo wakati alipokuwa katika mjadala maalumu huko White House uliokuwa na hamasa nyingi uliowashirikisha wanafunzi na wazazi walioathirika katika mashambulizi ya bunduki nchini Marekani.
Rais alisema huwenda pia wakaweka wanajeshi wa zamani katika shule zote jambo ambalo huwenda likatatua matatizo ya mashambulizi ya bunduki shuleni.
Wakati mjadala wa bunduki ukiendelea nchini Marekani, Rais Trump pia anafikiria kuwepo na kidhibiti cha umri kwa wanunuaji wa silaha kutoka miaka 18 hadi 21 ikiwemo silaha aina ya AR-15 iliyotumika kwenye shambulizi katika shule ya Florida jambo ambalo chama cha wamiliki wa silaha Marekani-NRA wanalipinga vikali.
Comments
Post a Comment