DC aagiza mbunge mwingine wa Chadema akamatwe


MBUNGE wa Chadema, katika jimbo la Tunduma, mkoani Mbeya, Frank Mwakajoka, amewekwa ndani muda huu kwa amri ya mkuu wa wilaya.
Mwakajoka ameswekwa rumande baada ya kuwapiga picha na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii, madiwani watatu wa chama hicho waliojiengua na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 
Wanadaiwa kupigwa picha na Mwakajoka, ni Ayub Mlimba ambaye alikuwa diwani wa kata ya (Mwaka Kati), Simon Mbukwa (Kaloleni) na Amos Nzunda (Mpemba).
Taarifa zinasema, tukio hilo lilitokea wakati madiwani hao walipoitwa na serikali kuhudhuria kikao cha bajeti cha halmashauri ya Mji Mdogo wa Tunduma, leo Jumatano.
“Hawa watatu wa nyuma ndio waliokuwa madiwani wa Chadema na ambao wamejiuzulu nafasi zao. Lakini leo wameitwa kwenye kikao cha bajeti cha Mji, huku wakiwa wamehama chama na kujiuzulu nafasi zao za udiwani,” ameeleza Mwakajoka katika moja ya ujumbe wake kwa wabunge wenzake.
Muda mfupi baadaye, mbunge huyo anaandika, “…na sasa nawekwa chini ya ulinzi na pia nakaa ndani kwa saa 48 kwa amri ya DC (mkuu wa wilaya).”
Baraza la madiwani la Tunduma linaundwa na Chadema; jambo ambalo linaifanya CCM ambacho ni chama cha upinzani, kutokuridhika na uamuzi huo wa wananchi.
Wote watatu walitangaza kuondoka Chadema, tarehe 6 Februari mwaka huu kwa madai yaleyale ya “kufurahishwa na utendaji kazi wa Rais John Magufuli.”

Comments

Popular posts from this blog

Diamond aibua jipya tuhuma za Hamisa Mobetto kupigwa na Bi. Sandrah

Idris Sultan ‘Mi Nina Kiingereza, Shilole una Nyumba Nani Anamcheka Mwenzie’

Sababu ya kuachiwa Babu Tale ni kuwa amri ya kumkamata yeye na ndugu yake Idd Shaban Taletale ilitolewa kimakosa

Zari Amkumbuka Ivan Katika Kumbukumbu Ya Kifo Chake....Leo Katimiza Mwaka Mmoja

Diamond Platnumz Apewa Gari Mpya na Uongozi wake wa Wasafi